Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 16:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Akalia, akasema, Baba Ibrahimu, unirehemu, umtume Lazaro, achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa maana naumia katika moto huu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Basi, akaita kwa sauti: ‘Babu Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Basi, akaita kwa sauti: ‘Babu Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Basi, akaita kwa sauti: ‘Babu Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Hivyo yule tajiri akamwita, ‘Baba Ibrahimu, nihurumie na umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake ndani ya maji aupoze ulimi wangu, kwa sababu nina maumivu makuu kwenye moto huu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Hivyo yule tajiri akamwita, ‘Baba Ibrahimu, nihurumie na umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake ndani ya maji aupoze ulimi wangu, kwa sababu nina maumivu makuu kwenye moto huu.’

Tazama sura Nakili




Luka 16:24
29 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake:


msiwaze moyoni kwamba, Tuna baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni ya kwamba Mungu anaweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.


Bali mimi nawaambiem, Killa amwoneae ndugu yake ghadhabu bila sababu, itampasa hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Haka, itampasa baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, itampasa jebannum ya moto.


Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini akienda kwao mmoja kutoka wafu watatubu.


Yesu akamwambia, Leo wokofu umefika nyumbani humu, kwa kuwa huyu nae ni mwana wa Ibrahimu.


Zaeni, bassi, matunda yapatanayo na toba wala msianze kusema ndani ya nafsi zenu, Tunae baba ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni, ya kwamba Mungu katika mawe haya aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.


Yesu akajibu akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, nae ni nani akuambiae, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, nae angalikupa maji yaliyo hayi.


walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.


Hatta siku ya mwisho, siku ile kubwa ya siku kuu, Yesu akasimama, akapaaza sauti yake, akinena, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.


na baba ya kutahiriwa, si kwa hao waliotahiriwa tu, bali kwa hao waliotahiriwa na kuzifuasa uyayo za imani yake baba yetu Ibrahimu aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa.


katika mwako wa moto, akiwalipa kisasi wao wasiomjua Mungu, nao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo;


Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Na huruma hujitukuza juu ya hukumu.


Kaangalieni jinsi moto mdogo uwasbavyo kuni nyingi sana. Nao ulimi ni moto, ulimwengu wa uovu. Ndio khabari ya ulimi katika viungo vyetu, huutia najis mwili wote, huliwasha moto gurudumu la maumbile, nao huwashwa moto na jehannum.


Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;


Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.


AKANIONYESHA mto wa maji ya uzima, wenye kungʼaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo