Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 16:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Bassi katika akhera akainua macho yake, akiwa katika adhabu, akamwona Ibrahimu yuko mbali, na Lazaro kifuani pake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Huyo tajiri, akiwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Huyo tajiri, akiwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Huyo tajiri, akiwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Kule Kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa kifuani mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Kule kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa karibu yake.

Tazama sura Nakili




Luka 16:23
26 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe Kapernaum, uliyeinuliwa hatta mbinguni, utashushwa hatta kuzimu: kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwako, ingalifanyika katika Sodom, ungalikuwapo hatta leo.


Na jicho lako likikukosesha, lingʼoe, ukalitupe mbali nawe; ni vyema zaidi kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jebannum ya moto.


Enyi nyoka, mazao wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehannum?


Bali mimi nawaambiem, Killa amwoneae ndugu yake ghadhabu bila sababu, itampasa hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Haka, itampasa baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, itampasa jebannum ya moto.


Jicho lako la kuume likikukosesha, lingʼoe ulitupe mbali nawe: kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehannum.


Wakapiga kelele, wakinena, Tuna nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu? Je, umekuja kutuadhibu kabla ya muhulla?


Akalia, akasema, Baba Ibrahimu, unirehemu, umtume Lazaro, achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa maana naumia katika moto huu.


maana nina ndugu watano; awashuhudie, wasije nao mahali hapa pa adhabu.


Alipomwona Yesu, akapiga kelele, akamwangukia, akasema kwa sauti kuu. Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuomba usiniadhibu.


U wapi, mauti, uchungu wako? Ku wapi, kaburi, kushinda kwako?


Kwa maana kama vile Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika mafungo ya giza, walindwe hatta ije hukumu;


Na yule Msingiziaji, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule nyama na yule nabii wa nwongo. Na wataumwa mchana na usiku hatta milele na milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo