Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 16:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Ikawa maskini akafa, akachukuliwa na malaika kifuani kwa Ibrahimu. Akafa na yule tajiri, akazikwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 “Basi, huyo maskini akafa, nao malaika wakamchukua, wakamweka karibu na Abrahamu. Na yule tajiri pia akafa, akazikwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 “Basi, huyo maskini akafa, nao malaika wakamchukua, wakamweka karibu na Abrahamu. Na yule tajiri pia akafa, akazikwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 “Basi, huyo maskini akafa, nao malaika wakamchukua, wakamweka karibu na Abrahamu. Na yule tajiri pia akafa, akazikwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 “Wakati ukafika yule maskini akafa, nao malaika wakamchukua akae pamoja na Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa na akazikwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 “Wakati ukafika yule maskini akafa, nao malaika wakamchukua akae pamoja na Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa na akazikwa.

Tazama sura Nakili




Luka 16:22
28 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.


Nae atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya panda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande mmoja wa mwisho wa mbinguni mpaka upande wa pili.


Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magbaribi, wataketi pamoja na Ibrabimu, na Isaak, na Yakob katika ufalme wa mbinguni;


Maana itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote akapata khasara ya roho yake?


Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo, wanakutaka roho yako. Nayo uliyojiwekea tayari yatakuwa ya nani?


akitamani kushibishwa na makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri: hatta mbwa nao huja, humramba vidonda vyake.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake.


Palikuwako mmoja wa wanafunzi wake, amemwegamia Yesu kifua chake, ambae Yesu alimpenda.


Na Petro akigeuka, akamwona mwanafunzi yule aliyependwa na Yesu akifuata; yeye ndiye aliyeegamia kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni na kusema, Bwana yu nani akusalitiye?


Hawo wote si roho zitumikazo, wakitumwa kuwakhudumu wale watakaourithi wokofu?


Bassi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye nae vivyo hivyo alishiriki yayo bayo, illi kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Shetani,


Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; na lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo nae tajiri atanyauka katika njia zake.


yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, illi, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe bayi kwa mambo ya haki; kwa kuchubuka kwake mliponywa.


Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Wa kheri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; na matendo yao yafuatana nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo