Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 16:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Akamwita, akamwambia, Nini hii nisikiayo juu yako? Toa khabari ya uwakili wako, maana huwezi tena kuwa wakili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Yule tajiri akamwita, akamwambia: ‘Ni mambo gani haya ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu, kwa maana huwezi kuwa karani tena.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Yule tajiri akamwita, akamwambia: ‘Ni mambo gani haya ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu, kwa maana huwezi kuwa karani tena.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Yule tajiri akamwita, akamwambia: ‘Ni mambo gani haya ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu, kwa maana huwezi kuwa karani tena.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Hivyo huyo tajiri akamwita na kumuuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayoyasikia kukuhusu? Toa taarifa ya usimamizi wako, kwa sababu huwezi kuendelea kuwa msimamizi.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Hivyo huyo tajiri akamwita na kumuuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayoyasikia kukuhusu? Toa taarifa ya usimamizi wako, kwa sababu huwezi kuendelea kuwa msimamizi.’

Tazama sura Nakili




Luka 16:2
23 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, nawaambieni, Killa neno lisilo maana, watakalolisema wana Adamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.


Kulipokuchwa, yule bwana wa mizabibu akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ijara yao, ukianzia wa mwisho hatta wa kwanza.


Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo, wanakutaka roho yako. Nayo uliyojiwekea tayari yatakuwa ya nani?


Bwana akasema, Nani, bassi, aliye wakili mwaminifu niwenye busara, ambae Bwana wake atamweka juu ya ntumishi wake wote, awape watu posho lao kwa saa yake?


TENA Yesu akawaambia wanafunzi wake, Kulikuwa na mtu tajiri, aliyekuwa na wakili; huyu akashitakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake.


Yule wakili akasema moyoni, Nifanyeje, kwa maana bwana wangu ananiondolea nwakili? Kulima siwezi; kuomba natahayari.


Bassi kama ni hivyo, killa mtu miongoni mwetu atatoa khabari za nafsi yake mbele za Mungu.


Kwa maana nimearifiwa khabari zenu, ndugu, na wale walio wa nyumba ya Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.


Tena inayohitajiwa katika mawakili, ndio mtu aonekane amini.


Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu ya Kristo, illi killa mtu apokee kadiri alivyotenda kwa mwili, vikiwa vyema au vikiwa vibaya.


Usiache kuitumia ile karama iliyo udani yako uliyopewa wewe kwa unabii, na kwa kuwekewa mikono ya wazee.


Dhambi za watu wengine ni dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhamhi zao zawafuata.


killa mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kukhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.


watakaotoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hayi na waliokufa.


Nikawaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele za Mungu; vitabu vikafunuliwa. Kitabu kingine kikafunuliwa, kilicho eha uzima, wafu wakahukumiwa kwa mambo ya matendo yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo