Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 16:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Akawaambia, Ninyi ndio watu wanaodai kuwa wenye haki mbele ya wana Adamu, lakini Mungu anajua mioyo yenu; kwa maana lililotukuka kwa wana Adamu, ni chukizo mbele ya Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Hapo akawaambia, “Nyinyi mnajifanya wema mbele ya watu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana kile kinachoonekana kuwa kitukufu mbele ya watu, Mungu anakiona kuwa takataka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Hapo akawaambia, “Nyinyi mnajifanya wema mbele ya watu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana kile kinachoonekana kuwa kitukufu mbele ya watu, Mungu anakiona kuwa takataka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Hapo akawaambia, “Nyinyi mnajifanya wema mbele ya watu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana kile kinachoonekana kuwa kitukufu mbele ya watu, Mungu anakiona kuwa takataka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Isa akawaambia, “Ninyi mnajionesha kuwa wenye haki mbele za wanadamu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana vile vitu ambavyo wanadamu wanavithamini sana, kwa Mungu ni machukizo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Isa akawaambia, “Ninyi mnajionyesha kuwa wenye haki mbele za wanadamu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana vile vitu ambavyo wanadamu wanavithamini sana, kwa Mungu ni machukizo.

Tazama sura Nakili




Luka 16:15
40 Marejeleo ya Msalaba  

Tena matendo yao yote huyatenda illi kutazamwa na watu: hupanua fulakteria zao, huongeza matamvna ya mavazi yao;


Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana: maana hujiumbua nyuso zao, illi waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao.


Bassi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika sunagogi na njiani, illi watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao.


Tena usalipo, usiwe kama wanafiki: kwa maana wapenda kusali wakisimama katika sunagogi na katika pembe za njia, illi waonekane na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao.


Nae akitaka kujifanya ana haki akamwambia Yesu, Na jirani yangu ni nani?


Bwana akamwambia, Sasa ninyi Mafarisayo mwasafisha kikombe na sabani kwa nje, lakini ndani yenu mmejaa unyangʼanyi ua uovu.


Yule Farisayo akasimama, akasali hivi kwa nafsi yake, Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine, wanyangʼanyi, wazinzi, waia kama na huyu mtoza ushuru.


Nawaambia ninyi, huyu alishuka nyumbani kwake amepata kibali kuliko yule: kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.


Akasema, Haya yote nimeyashika tangu ujana wangu.


Yesu akawaambia mfano huu watu waliojidhani nafsi zao kuwa wenye haki, wakiwadharau wengine wote.


Wakamvizia wakatuma wapelelezi, nao wakajifanya kuwa wenye haki, illi wamnase kwa neno lake, kusudi wamtie katika enzi na mamlaka ya liwali.


Wanakula nyumba za wajane: na kwa unafiki husali sala ndefu. Hawo watapokea hukumu iliyo kubwa zaidi.


na kwa sababu hakuwa na haja ya watu kushuhudia khabari za niwana Adamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwana Adamu.


Akamwambia marra ya tatu, Simon wa Yohana, Wanipenda mimi? Petro akahuzunika kwa kuwa alimwambia marra ya tatu, Wanipenda mimi? Akamwambia, Bwana, wewe unajua yote; unajua ya kuwa nakupenda. Yesu amwambia, Lisha kondoo zangu.


(Bassi huyu alinunua konde kwa ijara ya ndhalimu; akaanguka kifudifudi akapasuka, matumbo yake yote yakatoka.


Wakasali, wakasema, Wewe, Bwana, ujuae mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,


Na Mungu, ajuae mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vilevile kama alivyotupa sisi;


kwa maana hapana mwenye mwili atakaehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu, kwa matendo ya sheria: kwa maanii kujua dhambi kabisa huja kwa njia ya sharia.


Na yeye aichunguzae mioyo aijua nia ya Roho, ya kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.


Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


bali mtu wa moyoni asiyeonekana, katika jambo lisiloharibika; ni roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu kama mshipi, mpate kukhudumiana; kwa sababu Mungu hushindana na wenye kiburi, huwapa wanyenyekevu neema.


nami nitawaua watoto wake kwa manti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzae viuno na mioyo. Nami nitampa killa mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo