Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 16:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Hakuna mtumishi awezae kuwatumikia bwana wawili: maana au atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na Mamona.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 “Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au ataambatana na mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 “Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au ataambatana na mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 “Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au ataambatana na mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 “Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Kwa kuwa atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na Mali.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 “Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Kwa kuwa atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na Mali.”

Tazama sura Nakili

Luka 16:13
12 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo Yesu akamwambia, Nenda zako, Shetani: kwa maana imeandikwa, Utamsujudia Bwana Mungu wako, nae peke yake utamwabudu.

Hakuna mtu awezae kuwatumikia bwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja, na kumpenda wa pili; au atamshika mmoja, na kumtweza wa pili. Hamwezi kumtumikia Mungu na mamona.

Mtu asiye pamoja nami ni adui yangu: nae asiyekusanya pamoja nami hutapanya.

Mtu akija kwangu, nae hamehukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wanaume na wanawake, na uzima wake pia, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, nani atakaewapeni mali iliyo yenu wenyewe?

Na mimi nawaambia ninyi, Jifanyieni rafiki kwa mamona ya udhalimu, illi itakapopunguka wawakaribishe ninyi katika makao ya milele.

Yesu akamwambia, Msimkataze, kwa maana yeye asiye kinyume chetu ni upande wetu.

Enyi wazinzi, wanaume na wanawake, hamjui ya kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? bassi killa atakae kuwa rafiki wa dunia ajifanya kuwa adui wa Mungu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo