Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 16:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Bassi, ikiwa hamkuwa waaminifu katika mamona ya udhalimu, nani atakaewaaminisheni mali ya kweli?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Kama basi, nyinyi si waaminifu kuhusu mali mbaya za dunia, ni nani atakayewakabidhi zile mali za kweli?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Kama basi, nyinyi si waaminifu kuhusu mali mbaya za dunia, ni nani atakayewakabidhi zile mali za kweli?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Kama basi, nyinyi si waaminifu kuhusu mali mbaya za dunia, ni nani atakayewakabidhi zile mali za kweli?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Ikiwa hamkuwa waaminifu katika mali ya kidunia, ni nani atakayewaaminia mali ya kweli?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ikiwa hamkuwa waaminifu katika mali ya kidunia, ni nani atakayewaaminia mali ya kweli?

Tazama sura Nakili




Luka 16:11
9 Marejeleo ya Msalaba  

Hakuna mtu awezae kuwatumikia bwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja, na kumpenda wa pili; au atamshika mmoja, na kumtweza wa pili. Hamwezi kumtumikia Mungu na mamona.


Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu.


Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, nani atakaewapeni mali iliyo yenu wenyewe?


Na mimi nawaambia ninyi, Jifanyieni rafiki kwa mamona ya udhalimu, illi itakapopunguka wawakaribishe ninyi katika makao ya milele.


Yesu aliposikia haya, akamwambia, Neno moja hujalipata bado; viuze vitu vyote ulivyo navyo, ukawagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kiisha, njoo unifuate.


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


Sikihzeni, ndugu niwapendao, Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?


Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya nchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo