Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 15:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Akakasirika wala hakutaka kuingia: bassi, baba yake akatoka akamsihi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Huyo kijana mkubwa akawaka hasira hata akakataa kuingia nyumbani. Baba yake akatoka nje na kumsihi aingie.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Huyo kijana mkubwa akawaka hasira hata akakataa kuingia nyumbani. Baba yake akatoka nje na kumsihi aingie.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Huyo kijana mkubwa akawaka hasira hata akakataa kuingia nyumbani. Baba yake akatoka nje na kumsihi aingie.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 “Yule mwana mkubwa akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi baba yake akatoka nje na kumsihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 “Yule mwana mkubwa akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi baba yake akatoka nje na kumsihi.

Tazama sura Nakili




Luka 15:28
25 Marejeleo ya Msalaba  

Wakiisha kupokea, wakamnungʼunikia mwenye nyumba,


Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa.


Ee Yerusalemi, Yerusalemi, uwauae manabii na kuwapiga mawe wao waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hanikutaka!


Mafarisayo na wandishi wakanungʼunika, wakasema, Huyu hukaribisha wenye dhambi, hula pamoja nao.


Akamwambia, Ndugu yako amekuja: na baba yako amemchinja yule ndama aliyenona kwa sababu amempata yu mzima.


Akamjibu baba yake akamwambia, Tazama, mimi nimekutumikia hii miaka mingapi: wala sikukhalifu amri yako wakati wo wote wala hukunipa mimi mwana mbuzi wakati wo wote illi nifurahi pamoja na rafiki zangu.


na mataifa yote wakhubiriwe kwa jina lake toba na ondoleo la dhambi, kuanzia Yerusalemi.


Mafarisayo na waandishi wao wakawanungʼunikia wanafunzi wake, wakisema, Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?


Yule Farisayo aliyemwalika, alipoona haya akasema kimoyomoyo, akinena, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angalimjua huyu ni nani! na ni mwanamke gani anaemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi.


Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana.


Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watawa na watu wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paolo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.


Wayahudi wakalika toka Antiokia na Ikonio, wakawashawishi makutano hatta wakampiga mawe Paolo wakamhurura nje ya mji, wakidhani ya kuwa amekwisha kufa.


Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu.


Lakini nasema, Israeli hakufahamu? Hapo kwanza Musa anena, Nitawatieni moyo wa bidii kwa watu wasio taifa, Kwa taifa lisilo na fahamu nitawaghadhabisha.


Bassi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anakusihini kwa vinywa vyetu: twawaombeni kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.


wakituzuia tusiseme na mataifa wapate kuokolewa; illi watimize dhambi zao siku zote; lakini hasira imewafikia hatta mwisho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo