Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 15:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Lakini baba yake akawaambia watumishi wake, Ileteni joho iliyo bora, mkamvike: mpeni pete kwa kidole chake na viatu kwa miguu yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: ‘Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: ‘Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: ‘Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 “Lakini baba yake akawaambia watumishi, ‘Leteni upesi joho lililo bora sana, tieni pete kidoleni mwake na viatu miguuni mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 “Lakini baba yake akawaambia watumishi, ‘Leteni upesi joho lililo bora sana, tieni pete kidoleni mwake na viatu miguuni mwake.

Tazama sura Nakili




Luka 15:22
30 Marejeleo ya Msalaba  

Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili baada ya hayo kuitwa mwana wako.


Kamleteni yule ndama aliyenona, mkamchinje: tukale na kufurahi.


Bali mvaeni Bwana Yesu, wala msitafakari mahitaji ya mwili, nisije mkawasha tamaa zake.


ni haki ya Mungu, ipatwayo kwa kuwa na imani kwa Yesu Kristo, huja kwa watu wote, huwakalia watu wote waaminio.


Kwa kuwa hamkupokea roho ya utumwa uletao khofu, hali mlipokea roho ya kufanywa waua, kwa hiyo twalia, Abba, Baba.


Maana ninyi nyote mliobatizwa na kuingizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.


na kufungiwa miguu bali ya kuwa fayari tupatayo kwa Injili ya amani;


Nae alipewa kuvikwa kwa katani safi, ya fakhari, kwa maana katani hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.


Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae nitampa kula baadhi ya ile manna iliyofiehwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina, jina asilolijua mtu illa yeye aliyepewa.


Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya nchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona,


Wakapewa killa mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hatta itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao watakaouawa vile vile kama wao.


Baada ya haya nikaona, na tazama mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezae kuuhesabu, watu wa killa taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kiti kile cha enzi, na mbele za Mwana Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo