Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 14:32 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

32 Kama sivyo, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, yule mtu akiwa angali mbali.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Ikiwa hawezi, basi yule mwingine akiwa bado yuko mbali, yeye hutuma wajumbe na kuomba masharti ya amani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Kama hawezi, basi wakati yule mwingine akiwa bado yuko mbali, yeye hutuma ujumbe wa watu na kuomba masharti ya amani.

Tazama sura Nakili




Luka 14:32
11 Marejeleo ya Msalaba  

Patana na mshtaki wako upesi, wakati uwapo pamoja nae njiani; yule mshtaki asije akakupeleka kwa kadhi, kadhi akakutia mkononi mwa askari, ukatupwa kifungoni.


Akuombae, mpe; nae atakae kukopa kwako, usimpe kisogo.


Bassi, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa liwali, njiani ujitahidi kupatanishwa nae: asije akakukokota mbele ya kadhi, yule kadhi akakutia katika mikono ya askari, yule askari akakutupa gerezani.


Au mfalme gani, kama anakwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana nae anaemjia pamoja na watu elfu ishirini?


Bassi, kadhalika killa mmoja wenu asiyeviacha vitu vyote alivyo navyo hawezi kuwa mwanafunzi wangu.


Wenyeji wake wakanichukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatutaki mtu huyu atutawale.


Nae Herode aliwakasirikia sana watu wa Tʼuro na Sidon: wakamwendea kwa nia moja, na wakiislia kufanya urafiki na Blasto, mwenye kukitunza chumba cha mfalme cha kulalia, wakataka amani; kwa maana inchi yao ilipata riziki kwa inchi ya mfalme.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo