Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 14:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha assubuhi au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako walio na mali, wasije na wao wakakualika wewe, ukapata malipo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Halafu akamwambia na yule aliyemwalika, “Kama ukiwaandalia watu karamu mchana au jioni, usiwaalike rafiki zako au jamaa zako au jirani zako walio matajiri wasije nao wakakualika, nawe ukawa umelipwa kile ulichowatendea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Halafu akamwambia na yule aliyemwalika, “Kama ukiwaandalia watu karamu mchana au jioni, usiwaalike rafiki zako au jamaa zako au jirani zako walio matajiri wasije nao wakakualika, nawe ukawa umelipwa kile ulichowatendea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Halafu akamwambia na yule aliyemwalika, “Kama ukiwaandalia watu karamu mchana au jioni, usiwaalike rafiki zako au jamaa zako au jirani zako walio matajiri wasije nao wakakualika, nawe ukawa umelipwa kile ulichowatendea.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kisha Isa akamwambia yule aliyewaalika, “Uandaapo karamu ya chakula cha mchana au cha jioni, usialike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako walio matajiri tu. Ukifanya hivyo, nao wanaweza kukualika kwao, nawe ukawa umepata malipo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kisha Isa akamwambia yule aliyewaalika, “Uandaapo karamu ya chakula cha mchana au cha jioni, usialike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako walio matajiri tu. Ukifanya hivyo, wao nao wanaweza kukualika kwao, nawe ukawa umelipwa kile ulichofanya na kupata thawabu yako.

Tazama sura Nakili

Luka 14:12
13 Marejeleo ya Msalaba  

Maana mkiwapenda wanaowapendani, mwapata thawabu gani? Hatta watoza ushuru, je, nao hawafanyi yayo hayo?

Wenye njaa amewashibisha mema; Wenye mali amewaondoa mikono mitupu

Wakasikia jirani zake na jamaa zake ya kwamba Bwana amemwongezea rehema zake; wakafurahiwa pamoja nae.

Kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.

Bali ufanyapo karamu, wakaribishe maskini, vilema, viwete, vipofu: nawe utakuwa kheri:

Bassi, illi mlipe kadiri ile ile mliyopewa (nasema nanyi kama na watoto), mkunjuliwe mioyo na ninyi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo