Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 13:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Ee Yerusalemi, Yerusalemi, uwauae manabii na kuwapiga mawe wao waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hanikutaka!

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 “Yerusalemu! Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 “Yerusalemu! Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 “Yerusalemu! Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka!

Tazama sura Nakili

Luka 13:34
46 Marejeleo ya Msalaba  

Akawatuma watumishi wake wawaite walioalikwa kuja arusini: nao hawakutaka kuja.

nao waliosalia wakawakamata watumishi wake, wakawatenda jeuri, wakawana.

Akakasirika wala hakutaka kuingia: bassi, baba yake akatoka akamsihi.

watakuangusha chini, na watoto wako ndani yako; wasikuachie jiwe juu ya jiwe; kwa kuwa hukujua majira ya kujiliwa kwako.

Yesu akawageukia, akasema, Binti za Yerusalemi, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.

Ni yupi katika manabii ambae baba zenu hawakumwudhi? nao waliwaua wale waliotabiri khabari za kuja kwake yule mwenye haki; ambae ninyi sasa mmemsaliti mkamwua;

Wakampiga mawe Stefano, nae akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu.

NA Saul alikuwa akiona vema auawe. Siku ile kukatukia adha nyingi juu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wote wakatawanyika katika inchi ya Yahudi na Samaria, illa mitume.

Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wetu aliposulibiwa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo