Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 13:33 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

33 Illakini imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa, kwa maana haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Hata hivyo, kwa leo, kesho na kesho kutwa, ni lazima niendelee na safari yangu, kwa sababu si sawa nabii auawe nje ya Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Hata hivyo, kwa leo, kesho na kesho kutwa, ni lazima niendelee na safari yangu, kwa sababu si sawa nabii auawe nje ya Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Hata hivyo, kwa leo, kesho na kesho kutwa, ni lazima niendelee na safari yangu, kwa sababu si sawa nabii auawe nje ya Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Sina budi kuendelea na safari yangu leo, kesho na kesho kutwa: kwa maana haiwezekani nabii kufa mahali pengine isipokuwa Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Sina budi kuendelea na safari yangu leo, kesho na kesho kutwa: kwa maana haiwezekani nabii kufa mahali pengine isipokuwa Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Luka 13:33
10 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemi; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa makuhani wakuu na waandishi; nao watamhukumu afe;

Makutano wakanena, Huyu ni Yesu, yule nabii wa Nazareti ya Galilaya.

Nao hawakumkaribisha, kwa sababu nso wake ameuelekeza kwenda Yerusalemi.

Bassi Yesu hakutemhea tena kwa wazi kati ya Wayahudi, hali alitoka huko akaenda mahali karibu ya jangwa, hatta mji nitwao Efraim; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.

Yesu akajibu, Saa za mchana je si thenashara? Mtu akienda mchana hajikwai, kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.

Bassi Yesu akawaambia, Nuru ingali pamoja nanyi muda kitambo. Enendeni maadam mnayo ile nuru, giza lisije likawaweza; nae aendae gizani hajui aendako.

Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka nikaimalize kazi yake.

Yanipasa kuzifanya kazi zake aliyenipeleka maadam ni mchana: usiku waja, asipoweza mtu kufanya kazi.

khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.

Kwa maana wakaao Yerusalemi, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua huyu, wala sauti za manabii wanaosomwa killa sabato, wamezitimiza kwa kumhukumu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo