Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 13:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Akawaambia, Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba; kwa maana nawaambieni ya kwamba watu wengi watatafuta kuingia nao bawataweza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Yesu akawaambia, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; maana nawaambieni, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Yesu akawaambia, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; maana nawaambieni, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Yesu akawaambia, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; maana nawaambieni, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 “Jitahidini sana kuingia kupitia mlango mwembamba, kwa maana nawaambia wengi watajaribu kuingia, lakini hawataweza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Isa akawaambia, “Jitahidini sana kuingia kupitia mlango mwembamba, kwa maana nawaambia wengi watajaribu kuingia, lakini hawataweza.

Tazama sura Nakili




Luka 13:24
26 Marejeleo ya Msalaba  

Tangu siku za Yohana Mbatizaji hatta leo ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.


Mtu mmoja akamwambia, Bwana, wao wanaookolewa ni wachaehe?


Kwa hiyo kesheni killa wakati, mkiomba mpate kuhesabiwa kuwa mmestahili kuponea haya yote yatakayokuwa, na kusimama mahali penu mbele ya Mwana wa Adamu.


Enyi watoto wachanga, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta: na kama nilivyowaambia Wayahudi, ya kama, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja: sasa nawaambia na ninyi.


Kwa maana kuna wakati malaika hushuka akaiingia ile birika, akayatibua maji: bassi yeye aliyeingia kwanza baada ya maji kutibuliwa, akaponea ugonjwa wote uliokuwa umempata.


Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hatta uzima wa milele, Mwana wa Adamu atakachowapeni: maana huyu ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.


Mtanitafuta, wala hamtaniona; nami nilipo, ninyi hamwezi kuja.


Bassi Yesu akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta, na mtakufa katika dhambi yenu: niendako mimi, ninyi hamwezi kuja.


Kwa maana, wakiwa hawajui haki ya Mungu, na wakitaka kuithubutisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.


nami najitaabisha kwa hiyo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendae kazi ndani yangu kwa nguvu.


Bassi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, mtu ye yote asije akaanguka kwti mfano huo huo wa kuasi.


Kwa hivo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara wito wenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo