Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 13:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Bassi Bwana akamjibu, akasema, Ewe mnafiki, killa mmoja wenu je! hamfungui ngʼombe wake au punda wake mazizini siku ya sabato, akaenda nae kumnywesha?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Hapo Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng'ombe wake au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Hapo Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng'ombe wake au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Hapo Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng'ombe wake au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Lakini Bwana Isa akamjibu, “Enyi wanafiki! Je, kila mmoja wenu hamfungulii ng’ombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya Sabato?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Lakini Bwana Isa akamjibu, “Enyi wanafiki! Je, kila mmoja wenu hamfungulii ng’ombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya Sabato?

Tazama sura Nakili

Luka 13:15
16 Marejeleo ya Msalaba  

Waacheni hawo; ni vipofu, viongozi wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumhukia shimoni wote wawili.

Enyi wanafiki, ni vyema alivyotabiri Isaya katika khabari zenu, akinena,

Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.

Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, hali kwa ndani mmejaa unafiki na maasi.

Mnaflki, iondoe kwanza ile boriti katika jicho lako; ndipo utakapoona sana hatta kukiondoa kibanzi katika jicho la ndugu yako.

HUKO nyuma mkutano wa watu, watu elfu nyingi walipokusanyika hatta wakakanyagana, akaanza kuwaambia wanafunzi wake khassa, Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki.

Akajibu akawaambia, Nani wenu mwenye punda au ngʼombe ametumbukia kisimani, asiyemwondoa marra moja siku ya sabato?

Au wawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu, niache niondoe kibanzi kilichomo jichoni mwako, na wewe mwenyewe huioni boriti iliyomo jichoni mwako? Mnafiki, toa kwanza boriti iliyomo jichoni mwako, ndipo utakapoona vema kutoa kibanzi jichoni mwa ndugu yako.

Na Bwana alipomwona, akamhurumia, akamwambia, Usilie.

Yohana akaita wawili katika wanafunzi wake akawapeleka kwa Yesu, akisema, Wewe ndiye yule ajae, au tumtazamie mwingine?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo