Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 13:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 WAKATI huohuo walikuwapo watu wakimwarifu khabari za Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Wakati huo huo, kulikuwa na watu waliomwambia Isa habari za Wagalilaya ambao Pilato aliwaua, na damu ya hao watu akaichanganya na dhabihu yao waliyokuwa wanatoa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Wakati huo huo, kulikuwa na watu waliomwambia Isa habari za Wagalilaya ambao Pilato aliwaua, na damu ya hao watu akaichanganya na dhabihu yao waliyokuwa wanatoa.

Tazama sura Nakili

Luka 13:1
8 Marejeleo ya Msalaba  

ILIPOKUWA assubuhi, makuhani wakuu wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumfisha;

wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa liwali Pontio Pilato.

wakasema, Watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Si hawa wote wasemao Wagalilaya?

Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa kodi, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma yake, nae akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo