Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 12:58 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

58 Bassi, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa liwali, njiani ujitahidi kupatanishwa nae: asije akakukokota mbele ya kadhi, yule kadhi akakutia katika mikono ya askari, yule askari akakutupa gerezani.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

58 Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

58 Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

58 Maana kama mshtaki wako anakupeleka mahakamani, ingekuwa afadhali kwako kupatana naye mkiwa bado njiani, ili asije akakupeleka mbele ya hakimu, naye hakimu akakutoa kwa polisi, nao wakakutia ndani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

58 Ukiwa njiani na mshtaki wako kwenda kwa hakimu, jitahidi kupatana naye mkiwa njiani. La sivyo, atakupeleka kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa afisa, naye afisa atakutupa gerezani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

58 Uwapo njiani na mshtaki wako kwenda kwa hakimu, jitahidi kupatana naye mkiwa njiani. La sivyo, atakupeleka kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa afisa, naye afisa atakutupa gerezani.

Tazama sura Nakili

Luka 12:58
20 Marejeleo ya Msalaba  

Nae hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hatta atakapoilipa ile deni.

(maana anena, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokofu nilikusaidia; tazama, sasa ndio wakati uliokubalika sana; tazama, sasa ndio siku ya wokofu).

Kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni,

Walakini nitajitahidi, illi killa wakati baada ya kufariki kwangu mpate kuyakumbuka mambo haya.

Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia khabari ya wokofu wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikieni, illi niwaonye mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu marra moja tu.

Na ile miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa atoke kifungoni mwake:

Tufuate:

Matangazo

Matangazo