Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 12:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Illa nitawaonya mtakaemwogopa: Mwogopeni yule aliye na uweza baada ya kuua mtu kumtupa katika Jehannum: naam, nawaambieni, Mwogopeni yule.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Nitawaonesheni yule ambaye ni lazima kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua ana uwezo wa kumtupa mtu katika moto wa Jehanamu. Naam, ninawaambieni, mwogopeni huyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Nitawaonesheni yule ambaye ni lazima kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua ana uwezo wa kumtupa mtu katika moto wa Jehanamu. Naam, ninawaambieni, mwogopeni huyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Nitawaonesheni yule ambaye ni lazima kumwogopa: mwogopeni yule ambaye baada ya kuua ana uwezo wa kumtupa mtu katika moto wa Jehanamu. Naam, ninawaambieni, mwogopeni huyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua mwili, ana mamlaka ya kuwatupa motoni. Naam, nawaambia, mwogopeni huyo!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua mwili, ana mamlaka ya kuwatupa motoni. Naam, nawaambia, mwogopeni huyo!

Tazama sura Nakili




Luka 12:5
16 Marejeleo ya Msalaba  

Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho: afadhali mmwogopeni yule awezae kuangamiza mwili na roho pia katika jehannum.


Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake:


Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele.


Bali mimi nawaambiem, Killa amwoneae ndugu yake ghadhabu bila sababu, itampasa hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Haka, itampasa baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, itampasa jebannum ya moto.


Bali ninyi mwe macho: nimekwisha kuwaonyeni yote mbele.


mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizae kisasi cha haya yote, kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudu sana.


Ni jambo la kutisba kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hayi.


Kwa maana kama vile Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika mafungo ya giza, walindwe hatta ije hukumu;


akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, kamtukuzeni, maana saa ya hukumu yake imekuja. Kamsujuduni yeye aliyezifanya mbingu na inchi na bahari na chemchemi za maji.


Ni nani asiyekucha, Bwana, na kulitukuza jina lako? kwa kuwa wewe peke yako Mtakatifu: kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele yako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.


Mauti na Kuzimu wakatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo