Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 12:42 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

42 Bwana akasema, Nani, bassi, aliye wakili mwaminifu niwenye busara, ambae Bwana wake atamweka juu ya ntumishi wake wote, awape watu posho lao kwa saa yake?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

42 Bwana akajibu, “Ni nani, basi, aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wake ili awape chakula wakati ufaao?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

42 Bwana akajibu, “Ni nani, basi, aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wake ili awape chakula wakati ufaao?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

42 Bwana akajibu, “Ni nani, basi, aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wake ili awape chakula wakati ufaao?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

42 Isa akamjibu, “Ni yupi basi wakili mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamfanya msimamizi juu ya watumishi wake wote, ili awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

42 Isa akamjibu, “Ni yupi basi wakili mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamfanya msimamizi juu ya watumishi wake wote, ili awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa?

Tazama sura Nakili




Luka 12:42
29 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia, Kwa sababu hii, killa mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoae katika hazina yake vitu vipya na vya kale.


Kulipokuchwa, yule bwana wa mizabibu akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ijara yao, ukianzia wa mwisho hatta wa kwanza.


Yu kheri mtumishi yule ambae bwana wake ajapo atamkuta amefanya hivyo.


Na Bwana alipomwona, akamhurumia, akamwambia, Usilie.


Yohana akaita wawili katika wanafunzi wake akawapeleka kwa Yesu, akisema, Wewe ndiye yule ajae, au tumtazamie mwingine?


Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.


Lakini nikikawia, upate kujua sana jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu iliyo kanisa la Mungu aliye hayi, nguzo na msingi wa kweli.


Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha.


likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.


Maana imempasa askofu awe mtu asioshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mzoelea mvinyo, asiwe mpigaji, asiwe mpenda mapato ya aibu,


Watiini walio na mamlaka juu yenu, na kujinyenyekea kwao; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, illi wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.


Wakumbukeni wale waliokuwa na mamlaka juu yenu, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa maisha zao, iigeni imani yao.


Na Musa alikuwa mwaminifu katika nyumba yake yote kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa;


killa mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kukhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo