Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 12:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Lakini nawaambia ninyi rafiki zangu, Msiwaogope wao wauuao mwili na baada ya haya hawana neno la kutenda la zaidi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 “Nawaambieni nyinyi rafiki zangu: Msiwaogope wale wanaoua mwili, wasiweze kufanya kitu kingine zaidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 “Nawaambieni nyinyi rafiki zangu: Msiwaogope wale wanaoua mwili, wasiweze kufanya kitu kingine zaidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 “Nawaambieni nyinyi rafiki zangu: msiwaogope wale wanaoua mwili, wasiweze kufanya kitu kingine zaidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 “Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, lakini baada ya hilo hawawezi kufanya lolote zaidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 “Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, lakini baada ya hilo hawawezi kufanya lolote zaidi.

Tazama sura Nakili




Luka 12:4
20 Marejeleo ya Msalaba  

Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho: afadhali mmwogopeni yule awezae kuangamiza mwili na roho pia katika jehannum.


Hakima aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuweka uzima wake kwa ajili ya rafiki zake.


Lakini siyahesabu maisha yaugu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na khuduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.


Bassi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa ni watu wasio elimu, wasio maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.


wala hamwogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara wazi ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokofu, nao wa Mungu.


Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu ikahesabiwa kwake kuwa ni haki: nae aliitwa raliki wa Mungu.


Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki, in kheri; msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike;


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo