Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 12:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HUKO nyuma mkutano wa watu, watu elfu nyingi walipokusanyika hatta wakakanyagana, akaanza kuwaambia wanafunzi wake khassa, Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Wakati watu kwa maelfu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu aliwaambia kwanza wanafunzi wake, “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Wakati watu kwa maelfu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu aliwaambia kwanza wanafunzi wake, “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Wakati watu kwa maelfu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu aliwaambia kwanza wanafunzi wake, “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Wakati huo, umati mkubwa wa watu maelfu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Isa akaanza kuzungumza kwanza na wanafunzi wake, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Wakati huo, umati mkubwa wa watu maelfu, walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Isa akaanza kuzungumza kwanza na wanafunzi wake, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani, unafiki wao.

Tazama sura Nakili




Luka 12:1
18 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wenu, maana mfano wenu ni makaburi yasiyoonekana, na watu wapitao juu yao hawana khabari.


Enyi wanafiki, mwajua kuufasiri uso wa inchi na mbingu; imekuwaje, bassi, hamjui kuyafasiri majira haya?


IKAWA makutano walipomsonga, wakisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa akisimama kando ya ziwa la Genesareti:


Lakini khabari zake zikazidi kuenea, wakakutana makutano mengi kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.


Akatelemka pamoja nao, akasimama panapo uwanda, pamoja na kundi la wanafunzi wake, na kundi la watu waliotoka Yahudi wote, na Yerusalemi, na pwani ya Turo na Sidon, waliokuja wamsikilize na kuponywa maradhi zao;


Nao waliposikia wakamhimidi Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona kwamba Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati.


Kwa maana naliwapasha khabari ya mambo niliyoyapokea, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;


Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye tiayi, Yerusalemi wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,


Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki;


BASSI, mkiwekea mbali uovu wote na hila yote na unafiki na husuda na niasingizio yote,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo