Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 11:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Utupe leo riziki zetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa maana sisi nasi tunamsamehe killa mtu anaewiwa nasi. Usituingize majaribuni, hali utuokoe na yule mwovu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Utusamehe dhambi zetu, maana sisi tunawasamehe wote waliotukosea; wala usitutie katika majaribu.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Utusamehe dhambi zetu, maana sisi tunawasamehe wote waliotukosea; wala usitutie katika majaribu.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Utusamehe dhambi zetu, maana sisi tunawasamehe wote waliotukosea; wala usitutie katika majaribu.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa na sisi huwasamehe wote wanaotukosea. Wala usitutie majaribuni [bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu].’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa na sisi huwasamehe wote wanaotukosea. Wala usitutie majaribuni (bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu).’ ”

Tazama sura Nakili




Luka 11:4
31 Marejeleo ya Msalaba  

Vivyo hivyo na Baba yangu wa mbinguni atawatenda ninyi, kama ninyi kwa mioyo yenu hamkusamehe killa mtu ndugu yake makosa yake.


Kesheni, kaombeni, msije mkaingia majaribuni: Roho ina nia njema, bali mwili ni dhaifu.


Akawaambia, Nani kwenu aliye na rafiki akamwendea usiku wa manane akamwambia,


Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara katika Siloam, ukawaangamiza, mwadhani ya kuwa walikuwa wakosaji kuliko watu wote wakaao Yerusalemi?


Mbona mnielala? Ondokeni, mkaombe, msipate kuingia majaribuni.


Na wale juu ya mwamba ndio wale ambao, walisikiapo neno, hulipokea kwa furaha; na hawa hawana mizizi, huamini kwa kitambo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.


Siombi uwatoe katika ulimwengu, hali uwalinde na yule mwovu.


Jaribu halikuwapata ninyi, illa ya kadiri ya kibinadamu; na Mungu yu amini; hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, illi mweze kustahimili.


mkichukuliana, na kuachiliana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mtu; jinsi Kristo alivyowaachilieni, vivyo hivyo na ninyi.


Lakini Bwana ni mwaminifu, atakaewafanyeni imara na kuwaokoeni na yule mwovu.


Na Bwana ataniokoa na killa neno baya na kunihifadhi hatta uje ufalme wake wa milele.


Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Na huruma hujitukuza juu ya hukumu.


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Kwa kuwa ulilishika neno la uvumilivu wangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo