Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 11:36 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

36 Bassi, kama mwili wako wote nna nuru, tena kama hanna sehemu iliyo na giza, mwili wako utakuwa na nuru kabisa kama vile taa ikumulikiavyo kwa mwangaza wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

36 Basi, kama mwili wako wote una mwanga, bila kuwa na sehemu yoyote yenye giza, mwili huo utangaa kikamilifu kama vile taa inavyokuangazia kwa mwanga wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

36 Basi, kama mwili wako wote una mwanga, bila kuwa na sehemu yoyote yenye giza, mwili huo utangaa kikamilifu kama vile taa inavyokuangazia kwa mwanga wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

36 Basi, kama mwili wako wote una mwanga, bila kuwa na sehemu yoyote yenye giza, mwili huo utang'aa kikamilifu kama vile taa inavyokuangazia kwa mwanga wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

36 Basi ikiwa mwili wako wote umejaa nuru, bila sehemu yake yoyote kuwa gizani, basi utakuwa na nuru kama vile taa ikuangazavyo kwa nuru yake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

36 Basi ikiwa mwili wako wote umejaa nuru, bila sehemu yake yoyote kuwa gizani, basi utakuwa na nuru kama vile taa ikuangazavyo kwa nuru yake.”

Tazama sura Nakili




Luka 11:36
22 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia, Kwa sababu hii, killa mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoae katika hazina yake vitu vipya na vya kale.


Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya kibaba, bali juu ya kibao cha kuwekea taa; nayo yaangaza wote waliomo nyumbani.


Angalia bassi, ile nuru iliyo ndani yako isije ikawa giza.


Hatta alipokuwa akisema, Farisayo mmoja akamwita ale chakula cha assubuhi kwake: akaingia, akaketi.


Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.


illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu;


Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; kwa neema mkimwimbia Bwana mioyoni mwenu.


Lakini chakula kigumu in cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.


Lakini aliyeitazama sharia kamilifu ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyu atakuwa wa kheri katika kutenda kwake.


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo