Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 11:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Taa ya mwili ni jicho, bassi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote nna nuru, lakini jicho lako likiwa ovu, mwili wako nao una giza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Jicho lako ni taa ya mwili wako; likiwa zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga. Jicho lako likiwa bovu, na mwili wako pia utakuwa katika giza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Jicho lako ni taa ya mwili wako; likiwa zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga. Jicho lako likiwa bovu, na mwili wako pia utakuwa katika giza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Jicho lako ni taa ya mwili wako; likiwa zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga. Jicho lako likiwa bovu, na mwili wako pia utakuwa katika giza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Jicho lako ni taa ya mwili wako. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote pia umejaa nuru. Lakini kama jicho ni bovu, mwili wako wote pia umejaa giza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Jicho lako ni taa ya mwili wako. Kama jicho lako ni zima, mwili wako wote pia umejaa nuru. Lakini kama jicho ni bovu, mwili wako wote pia umejaa giza.

Tazama sura Nakili




Luka 11:34
28 Marejeleo ya Msalaba  

illi wakitazama watazame, wasione; na wakisikia wasikie, wasifahamu; wasije wakageuka, wakasamehewa dbambi zao.


wizi, uuaji, tamaa mbaya, hila, jeuri, kijicho, matukano, kiburi, upumbafu.


Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? wala hamkumbuki?


Angalia bassi, ile nuru iliyo ndani yako isije ikawa giza.


Bassi, angalia, mkono wa Bwana ni juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda kitambo. Marra kiwi kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.


Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kupokea chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,


uwafumhue macho yao, waiache giza na kuielekea nuru, na waziache nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu, na wapate masamaha ya dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu.


Hwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa unyofu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na khassa kwenu ninyi.


Lakini naogopa; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikara zenu, mkauacha unyofu wenu kwa Kristo.


ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awapeni roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye:


Watumwa, watiini walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili kana kwamba ni kumtii Kristo, kwa khofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo,


Ninyi watumwa, watiini wao ambao kwa niwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wana Adamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimeha Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo