Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 11:31 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

31 Malkia wa kusini atafufuliwa siku ile ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nae atawahukumu; kwa sababu yeye alikuja kutoka ncha za dunia illi kuisikia hekima ya Sulemani; na hapa pana khabari kubwa kuliko Sulemani.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atakihukumu kwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni na kumbe hapa pana mkuu kuliko Solomoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atakihukumu kwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni na kumbe hapa pana mkuu kuliko Solomoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atakihukumu kwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni na kumbe hapa pana mkuu kuliko Solomoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kuwahukumu watu wa kizazi hiki. Kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Sulemani. Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kuwahukumu watu wa kizazi hiki. Kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Sulemani. Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.

Tazama sura Nakili

Luka 11:31
11 Marejeleo ya Msalaba  

Malkia wa kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nae atakihukumu: maana yeye alikuja kutoka pande za mwisho za ulimwengu asikie hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.

Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama hua, sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe mwana wangu, mpendwa wangu, ndiwe unipendezae.

Sauti ikatoka katika lile wingu ikasema, Huyu ni Mwana wangu, mpendwa wangu, msikieni yeye.

Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikae torati, hatakuhukumu wewe, uliye na maandiko na kutahiriwa, ukaikhalifu torati?

Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo