Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 11:29 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

29 Makutano walipokuwa wakimkusanyikia akaanza kunena, Kizazi hiki ni kizazi kibaya: chatafuta ishara: wala hakitapewa ishara illa ishara ya nabii Yunus.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu akawaambia, “Kizazi hiki ni kizazi kiovu. Kinataka ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya Yona.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu akawaambia, “Kizazi hiki ni kizazi kiovu. Kinataka ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya Yona.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu akawaambia, “Kizazi hiki ni kizazi kiovu. Kinataka ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya Yona.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Umati wa watu walipokuwa wanazidi kuongezeka, Isa akaendelea kusema, “Hiki ni kizazi kiovu. Kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ya Yona.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Umati wa watu ulipokuwa unazidi kuongezeka, Isa akaendelea kusema, “Hiki ni kizazi kiovu. Kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ya Yona.

Tazama sura Nakili




Luka 11:29
19 Marejeleo ya Msalaba  

Hatta akiona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, akawaambia, Uzao wa nyoka, nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu ijayo?


Maana killa mtu atakaenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha zina na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya yeye atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.


Wengine kwa kumjaribu wakataka ishara ya mbinguni.


illi kwa kizazi hiki itakwe damu ya manabii wote ilivomwagika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu;


HUKO nyuma mkutano wa watu, watu elfu nyingi walipokusanyika hatta wakakanyagana, akaanza kuwaambia wanafunzi wake khassa, Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki.


Yesu akajibu akasema, Enyi kizazi kisichoamini na upofu, nikae nanyi hatta hui? Mlete mwana wako hapa.


Bassi Wayahudi wakajibu wakamwambia, Ishara gani utuonyeshayo, iwapo unafanya haya?


Wakamwambia, Unafanya ishara gani bassi illi tuone tukaamini? Unatenda kazi gani?


Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo