Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 11:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Akawaambia, Msalipo, semeni: Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako takatifu litukuzwe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Yesu akawaambia, “Mnaposali, semeni: ‘Baba! Jina lako litukuzwe; ufalme wako ufike.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Yesu akawaambia, “Mnaposali, semeni: ‘Baba! Jina lako litukuzwe; ufalme wako ufike.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Yesu akawaambia, “Mnaposali, semeni: ‘Baba! Jina lako litukuzwe; ufalme wako ufike.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Akawaambia, “Mnapoomba, semeni: “ ‘Baba yetu [uliye mbinguni], jina lako litukuzwe, ufalme wako uje. [ Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.]

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Akawaambia, “Mnapoomba, semeni: “ ‘Baba yetu (uliye mbinguni), jina lako litukuzwe, ufalme wako uje. (Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.)

Tazama sura Nakili




Luka 11:2
45 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi killa mtu atakaenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.


Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Vivi hivi nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wakamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.


IKAWA alipokuwa mahali fullani, anasali, alipokoma, mmoja katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali kama Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.


kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu: Neema iwe kwenu na imani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwaua Yesu Kristo.


Kwa kuwa hamkupokea roho ya utumwa uletao khofu, hali mlipokea roho ya kufanywa waua, kwa hiyo twalia, Abba, Baba.


Neema na iwe kwenu, na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.


Neema iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu illi atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu:


Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwaua Yesu Kristo.


Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo.


Sasa Mungu, Baba yetu, atukuzwe milele na milele. Amin.


kwa ndugu watakatifu na waaminifu, walio ndani ya Kolossai, Neema iwe kwenu na imani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.


PAOLO, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathessaloniki, katika Mungu Baba, na Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.


wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;


Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,


Malaika wa saha akapiga baragumu, pakawa sauti kuu katika mbingu, zikisema, Falme za dunia zimekwisha kuwa ufalme na Mungu na wa Kristo wake, nae atamiliki hatta milele na milele.


Ni nani asiyekucha, Bwana, na kulitukuza jina lako? kwa kuwa wewe peke yako Mtakatifu: kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele yako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.


Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Halleluya; kwa kuwa Bwana Mungu Mwenyiezi amemiliki.


Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo