Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 11:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Bassi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, Baba aliye mbinguni, je! hatazidi na kuwapa wote wamwombao Roho Mtakatifu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Kama nyinyi, ingawa ni waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho Mtakatifu wale wanaomwomba.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Kama nyinyi, ingawa ni waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho Mtakatifu wale wanaomwomba.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Kama nyinyi, ingawa ni waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho Mtakatifu wale wanaomwomba.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa Roho Mtakatifu wa Mungu wale wamwombao!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Basi ikiwa ninyi mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa Roho wa Mwenyezi Mungu wale wamwombao!”

Tazama sura Nakili




Luka 11:13
30 Marejeleo ya Msalaba  

Vivi hivi nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wakamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.


illi mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni: maana yeye jua lake huwazushia waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.


Kwa kuwa wako ni ufalme, na nguvu, na utukufu, hatta milele. Amin. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nanyi.


Lakini Mungu akiyavika hivi majani ya mashamba, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je, hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?


Kwa maana haya yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji haya yote.


Kama ninyi, bassi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! si zaidi Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wamwombao?


au akimwomba yayi, atampa nge?


Akawaambia, Msalipo, semeni: Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako takatifu litukuzwe.


Bassi Mungu je! hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, nae ni mvumilivu kwao? Nawaambieni atawapatia haki upesi.


Yesu akajibu akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, nae ni nani akuambiae, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, nae angalikupa maji yaliyo hayi.


Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


Kwa maana ikiwa kwa kuteleza mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.


Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai neno jema: kwa kuwa kutaka ni katika uwezo wangu, bali kutenda lililo jema sipati.


Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja nae?


Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, maasi, tumedanganywa, tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukienenda katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo