Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 10:42 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

42 lakini kuna haja ya kitu kimoja tu, na Mariamu ameichagua sehemu iliyo njema, ambayo hataondolewa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

42 Kitu kimoja tu ni muhimu. Maria amechagua kitu bora zaidi ambacho hakuna mtu atakayemnyanganya.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

42 Kitu kimoja tu ni muhimu. Maria amechagua kitu bora zaidi ambacho hakuna mtu atakayemnyanganya.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

42 Kitu kimoja tu ni muhimu. Maria amechagua kitu bora zaidi ambacho hakuna mtu atakayemnyang'anya.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

42 Lakini kunahitajika kitu kimoja tu. Mariamu amechagua kile kilicho bora, wala hakuna mtu atakayemwondolea.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

42 Lakini kunahitajika kitu kimoja tu. Maria amechagua kile kilicho bora, wala hakuna mtu atakayemwondolea.”

Tazama sura Nakili




Luka 10:42
36 Marejeleo ya Msalaba  

Maana itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote akapata khasara ya roho yake?


Nae alikuwa na ndugu mwanamke aitwae Mariamu, nae alikuwa ameketi miguuni pa Yesu, akasikia maneno yake.


IKAWA alipokuwa mahali fullani, anasali, alipokoma, mmoja katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali kama Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.


Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo, wanakutaka roho yako. Nayo uliyojiwekea tayari yatakuwa ya nani?


Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu.


Akamwita, akamwambia, Nini hii nisikiayo juu yako? Toa khabari ya uwakili wako, maana huwezi tena kuwa wakili.


Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kuwa ulipokea mema yako katika maisha yako, na Lazaro kadhalika mabaya; lakini sasa yeye yupo hapa anafarajiwa, nawe unanmizwa.


Yesu aliposikia haya, akamwambia, Neno moja hujalipata bado; viuze vitu vyote ulivyo navyo, ukawagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kiisha, njoo unifuate.


Jihadharini, bassi, jinsi msikiavyo. Maana yeye aliye na kitu, atapewa: nae asiye na kitu ataondolewa hatta kitu kile ambacho anaonekana kuwa anacho.


BASSI mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mtu wa mji wa Mariamu na Martha dada yake.


na watu wengi katika Wayahudi wamekuja kwa Martha na Mariamu, illi kuwafariji kwa ajili ya ndugu yao.


Bassi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akaifuta miguu yake kwa nywele zake; nyumha ikajaa harufu ya yale marhamu.


Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.


Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hatta uzima wa milele, Mwana wa Adamu atakachowapeni: maana huyu ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.


Tena mkiwagawia maskini mali yangu yote, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo