Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 10:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Saa ileile Yesu akashangilia katika Roho, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na busara mambo haya, ukawafunulia watoto wachanga: Naam, Baba, kwa maana ndivyo vilivyokuwa vinapendeza mbele yako.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Saa ileile, Yesu akafurahi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akasema, “Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, maana umewaficha wenye hekima na wenye elimu mambo haya, ukawafumbulia wadogo. Naam, Baba, ndivyo ilivyokupendeza.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Saa ileile, Yesu akafurahi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akasema, “Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, maana umewaficha wenye hekima na wenye elimu mambo haya, ukawafumbulia wadogo. Naam, Baba, ndivyo ilivyokupendeza.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Saa ileile, Yesu akafurahi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akasema, “Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, maana umewaficha wenye hekima na wenye elimu mambo haya, ukawafumbulia wadogo. Naam, Baba, ndivyo ilivyokupendeza.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Wakati huo Isa akashangilia katika Roho wa Mungu, akasema, “Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo. Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Wakati huo Isa akashangilia katika Roho wa Mwenyezi Mungu, akasema, “Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo. Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza.

Tazama sura Nakili

Luka 10:21
29 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu, akamwambia, U kheri Simon bar Yunus; kwa kuwa nyama na damu hazikukufunulia haya, bali Baba yangu aliye mbinguni.

wakamwambia, Wasikia hawa wanenavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa?

Hatta akiona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, akawaambia, Uzao wa nyoka, nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu ijayo?

Amin, nawaambieni, Yeye yote asiyeukubali nfalme wa Mungu kama mtoto mchanga hatauingia kabisa.

Bassi amwonapo humweka mabegani mwake, akifurahiwa.

Bassi, aionapo, huwaita shoga zake na jirani zake, hunena, Furahini pamoja nami, kwa maana nimeiona ile mpia niliyoipoteza.

Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.

Ijapokuwa injili yetu imesetirika, imesetirika kwao wanaopotea;

ambae ndani yake sisi tumepata urithi, tukichaguliwa tangu awali kwa kusudi lake yeye afanyae yote kwa shauri la nia yake;

Kwa kuwa ametuchagua tangu zamani illi tufanywe waua wake yeye kwa njia ya Yesu Kristo, kwa mapenzi ya nia yake,

Tufuate:

Matangazo

Matangazo