Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 10:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Awasikiae ninyi, anisikia mimi, nae awakataae ninyi, anikataa mimi; nae anikataae mimi amkataa yeye aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Halafu akasema, “Anayewasikiliza nyinyi, ananisikiliza mimi; na anayekataa kuwapokea nyinyi, anakataa kunipokea mimi. Na yeyote anayekataa kunipokea, anakataa kumpokea yule aliyenituma.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Halafu akasema, “Anayewasikiliza nyinyi, ananisikiliza mimi; na anayekataa kuwapokea nyinyi, anakataa kunipokea mimi. Na yeyote anayekataa kunipokea, anakataa kumpokea yule aliyenituma.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Halafu akasema, “Anayewasikiliza nyinyi, ananisikiliza mimi; na anayekataa kuwapokea nyinyi, anakataa kunipokea mimi. Na yeyote anayekataa kunipokea, anakataa kumpokea yule aliyenituma.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 “Yeye awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi; naye awakataaye ninyi amenikataa mimi. Lakini yeye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 “Yeye awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi; naye awakataaye ninyi amenikataa mimi. Lakini yeye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.”

Tazama sura Nakili

Luka 10:16
17 Marejeleo ya Msalaba  

Awapokeae ninyi, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenituma.

Na ye yote atakaepokea kitoto kimoja mfano wa hiki kwa jina langu, anipokea mimi:

Mtu akimpokea kitoto kimoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, hanipokei mimi, bali yeye aliyenituma.

akawaambia, Killa mtu atakaempokea kitoto hiki kwa jina langu, anipokea mimi, na killa mtu atakaenipokea mimi, ampokea yeye aliyenituma. Maana yeye aliye mdogo miongoni mwenu ninyi nyote, huyu atakuwa mkubwa.

Yesu akapaaza sauti yake akasema, Aniaminiye mimi, haniamini mimi, bali yeye aliyenipeleka.

Anikataae mimi, asiyekubali maneno yangu, anae amhukumuye: neno lile nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeae ye yote nimpelekae, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenipeleka.

Ulipokuwa kwako, haukuwa mali yako? Na ulipokuwa umekwisha kuuzwa haukuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hatta ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uwongo mwana Adamu, bali Mungu.

na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Yesu Kristo.

Bassi yeye anaekataa, hakatai mwana Adamu bali Mungu, anaewapeni Roho yake Mtakatifu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo