Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 1:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Nao wote wawili wenye haki mbele ya Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na hukumu zake zote bila lawama.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Zakaria na Elizabeti mkewe wote walikuwa watu wanyofu mbele za Mungu, wakizishika amri zote za Mwenyezi Mungu na maagizo yote bila lawama.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Zekaria na Elizabeti mkewe wote walikuwa watu wanyofu mbele za Mwenyezi Mungu, wakizishika amri zote za Bwana Mwenyezi Mungu na maagizo yote bila lawama.

Tazama sura Nakili




Luka 1:6
33 Marejeleo ya Msalaba  

Nao walikuwa hawana mtoto; maana Elizabeti alikuwa tassa, nao wote wawili wazec sana.


Akawaambia, Ninyi ndio watu wanaodai kuwa wenye haki mbele ya wana Adamu, lakini Mungu anajua mioyo yenu; kwa maana lililotukuka kwa wana Adamu, ni chukizo mbele ya Mungu.


Bassi kulikuwako mtu katika Yerusalemi, jina lake Sumeon; na yule mtu mwenye haki, mtawa, akitazamia faraja ya Israeli: na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja nae.


Maana Daud amtaja khabari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko mkono wangu wa kuume, nisitikisike.


PAOLO akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu, mimi kwa nia safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hatta leo hivi.


Nami ninajizoeza katika neno hili kuwa na dhamiri isiyo na khatiya mbele ya Mungu na mbele ya watu.


Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele ya Mungu.


illi wema uagizwao na torati utimizwe ndani yetu, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.


Tena nawasifu, ndugu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale niliyowatolea vile vile kama nilivyowatolea.


Hwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa unyofu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na khassa kwenu ninyi.


mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala ndanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, na kilichopotoka; kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, mkishika neno la uzima;


katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, illi awalete ninyi mbele zake, watakatifu, hamna mawaa wala lawama,


apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.


Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.


Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa killa atendae haki amezaliwa nae.


Na hivi twajua ya kuwa tumemjua, ikiwa tunashika amri zake.


Wanangu, mtu asikudanganyeni; afanyae haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo