Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 1:41 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

41 Ikawa Elizabeti alipoisikia salamu ya Mariamu, mtoto mchanga akaruka ndani ya tumbo lake; Elizabeti akajazwa Roho Mtakatifu, akapaaza sauti yake kwa nguvu, akasema,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

41 Mara tu Elisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga tumboni mwake Elisabeti akaruka. Naye Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

41 Mara tu Elisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga tumboni mwake Elisabeti akaruka. Naye Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

41 Mara tu Elisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga tumboni mwake Elisabeti akaruka. Naye Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

41 Naye Elizabeti aliposikia salamu ya Mariamu, mtoto aliyekuwa tumboni mwake akaruka. Elizabeti akajazwa na Roho wa Mungu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

41 Naye Elizabeti aliposikia salamu ya Mariamu, mtoto aliyekuwa tumboni mwake akaruka. Elizabeti akajazwa na Roho wa Mwenyezi Mungu,

Tazama sura Nakili




Luka 1:41
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maani atakuwa mkuu mbele ya Mungu, hatakunywa divai wala kileo: nae atajazwa Roho Mtakatifu hatta tangu tumbo la mama yake.


Akaingia nyumbani kwa Zakaria, akamwamkia Elizabeti.


Umebarikiwa wewe katika wanawake, na uzao wa tumbo lako umebarikiwa.


Kwa maana sauti ya salamu yako ilipoingia masikioni mwangu, mtoto mchanga aliruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.


Zakaria babae akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akinena,


NA Yesu, akijaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani: akaongozwa na Roho kwenda jangwani, akijaribiwa na Shetani muda wa siku arubaini.


Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha mbalimbali, kama Roho alivyowajalia kutamka.


Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia,


Bassi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, illi tuwaweke juu ya jambo hili:


Nae akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama mkono wa kuume wa Mungu.


Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Saul, Bwana amenipeleka, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.


Tena msilevye kwa mvinyo, kwa kuwa haina kiasi, bali mjazwe Roho;


Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo