Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 1:35 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

35 Malaika akajibu, akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia, na nguvu zake Aliye juu zitakutilia kivuli: kwa biyo kitakachozaliwa kitakwitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Malaika akamjibu, “Roho wa Mungu atakujilia juu yako, nazo nguvu zake Yeye Aliye Juu Sana zitakufunika kama kivuli. Kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Malaika akamjibu, “Roho wa Mwenyezi Mungu atakujilia juu yako, nazo nguvu zake Yeye Aliye Juu Sana zitakufunika kama kivuli. Kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu.

Tazama sura Nakili




Luka 1:35
26 Marejeleo ya Msalaba  

Na kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipoposwa na Yusuf, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.


Alipokuwa akifikiri haya, malaika wa Bwana akamtokea katika udoto, akisema, Yusuf, mwana wa Daud, usikhofu kumchukua Mariamu mke wako, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.


Nao waliokuwa ndani ya chombo wakamwendea, wakamsujudia, wakinena, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.


Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.


Mjaribu akamjia akasema, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.


Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu;


akinena, Tʼuna nini nawe, Yesu Mnazareti? umekuja kutuangamiza? Nakutambua wewe, Mtakatifu wa Mungu.


kwa mwanamke bikira aliyekuwa ameposwa na mume, jina lake Yusuf, wa nyumba ya Daud; na jina la yule mwanamke Mariamu.


Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili; kwa maana simjui mume?


Na tazama, nae Elizabeti jamaa yako, ana mimba ya mtoto mume katika uzee wake: na mwezi hun wa sita kwake yeye aliyekwitwa tassa:


Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.


Nathanaeli akajibu, akamwambia, Rabbi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe mfalme wa Israeli.


lakini hizi zimeandikwa mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.


Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji: yule tawashi akasema, Yanizuia nini nisibatizwe?


na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo; Yesu Kristo Bwana wetu,


Nimesulibiwa pamoja na Kristo, illakini ni hayi; wala si mimi tena, bali Kristo yu hayi ndani yangu; na uhayi nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.


ambazo sisi nasi sote tuliziendea, hapo zamani, katika tamaa za mwili wetu, tukiyatimiza mapenzi ya mwili wetu na ya nia zetu, tukawa kwa tabia yetu watoto wa ghadhabu kama na hao wengine.


Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuyachukua mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijuribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo