Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 1:32 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

32 Huyu atakuwa mkuu, atakwitwa Mwana wake Aliye juu; na Bwana Mungu atampa kiti cha Daud baba yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Yeye atakuwa mkubwa na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Yeye atakuwa mkubwa na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Yeye atakuwa mkubwa na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Mwenyezi Mungu atampa kiti cha utawala cha Daudi baba yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. bwana Mwenyezi Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake.

Tazama sura Nakili




Luka 1:32
39 Marejeleo ya Msalaba  

KITABU eba ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daud, mwana wa Ibrahimu.


Malkia wa kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nae atakihukumu: maana yeye alikuja kutoka pande za mwisho za ulimwengu asikie hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.


Yesu akaja kwao, akasema nao, akinena, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na juu ya dunia.


Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


Lakini akanyamaza, wala hakujibu neno. Knbani mkuu akamwuliza tena, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake aliye Mtukufu?


akalia kwa sauti kuu akanena, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi, uniapie kwa Mungu kwamba hutaniadhibu.


Kwa maani atakuwa mkuu mbele ya Mungu, hatakunywa divai wala kileo: nae atajazwa Roho Mtakatifu hatta tangu tumbo la mama yake.


Malaika akajibu, akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia, na nguvu zake Aliye juu zitakutilia kivuli: kwa biyo kitakachozaliwa kitakwitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.


Na wewe nawe, Mtoto, utakwitwa nabii wake Aliye juu: Kwa maana utatangulia mbele ya uso wake Bwana ufanyize njia zake;


Yohana akajibu, akawaambia wote, Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba mimi sistahili kumfungulia ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto:


Bali wapendeni adui zenu, katendeni kwa ihsani, kopeshani, bali kutumaini kupata kitu tena: na thawabu yenu itakuwa nyingi, na mtakuwa wana wa Aliye juu sana; kwa sabahu Yeye yu mwema kwa watu wasio na shukrani, na waovu.


Bassi makutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hatta milele: nawe wanenaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?


Nasi tumeamini, tena tumejua ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi.


Akamfuata Paolo na sisi, akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kutukhubiri njia ya wokofu.


Bassi kwa kuwa nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake kwa jinsi ya kiwiliwili atamwinua Kristo, akae katika kiti chake cha enzi; yeye mwenyewe


Bassi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.


Illakini yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizofanyika kwa mikono, kama vile asemavyo nabii:


na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo; Yesu Kristo Bwana wetu,


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Filadelfia andika; Haya ayanena yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daud, mwenye kufungua wala hapana afungae, nae afunga wala hapana afuuguae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo