Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 1:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Nae atatangulia mbele ya uso wake, mwenye roho ya Eliya, na nguvu zake, kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na kuwageuza maasi waelekee akili zao wenye haki; illi kumfanyia tayari Bwana watu waliotengenezwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama ya Elia. Atawapatanisha kina baba na watoto wao; atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu, na hivyo amtayarishie Bwana watu wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama ya Elia. Atawapatanisha kina baba na watoto wao; atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu, na hivyo amtayarishie Bwana watu wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama ya Elia. Atawapatanisha kina baba na watoto wao; atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu, na hivyo amtayarishie Bwana watu wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Naye atatangulia mbele za Mwenyezi Mungu katika roho na nguvu ya Ilya, ili kuigeuza mioyo ya baba kuwaelekea watoto wao, na wasiotii warejee katika hekima ya wenye haki, ili kuwaweka tayari watu walioandaliwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Naye atatangulia mbele za Bwana katika roho na nguvu ya Ilya, ili kuigeuza mioyo ya baba kuwaelekea watoto wao, na wasiotii warejee katika hekima ya wenye haki, ili kuliweka tayari taifa lililoandaliwa kwa ajili ya Bwana Mwenyezi.”

Tazama sura Nakili




Luka 1:17
38 Marejeleo ya Msalaba  

Na ikiwa mantaka kukubali, yeye ndiye Elia atakaekuja.


Kwa sababu Yohana alimwambia, Ni haramu kwako kukaa uae.


Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti yake apigae mbin jangwani, Itengenezeni njia ya Bwana, Nyosheni mapito yake.


Yohana mwenyewe alikuwa na mavazi yake ya singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.


Na wengi katika wana wa Israeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.


Na wewe nawe, Mtoto, utakwitwa nabii wake Aliye juu: Kwa maana utatangulia mbele ya uso wake Bwana ufanyize njia zake;


waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.


Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.


Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake.


Marra nikatuma watu kwako, nawe umefanya vyema kuja. Bassi sasa sisi sote tupo hapa mbele za Mungu, tupate kuyasikiliza maneno yote uliyoamriwa na Mungu.


tena ajulishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema alivyovitengeneza tangu zamani, vipate utukufu,


mkimshukuru Baba, aliyetustahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru;


Bassi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hawa atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa killa kazi iliyo njema.


Bali ninyi m mzao mteule, ukubani wa kifaume, taifa takatifu, watu wa milki, mpate kutangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, illi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibishwe mbele zake katika kuja kwake.


Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo