Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 1:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mke wako Elizabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Lakini malaika akamwambia, “Zakaria, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Lakini malaika akamwambia, “Zakaria, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Lakini malaika akamwambia, “Zakaria, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Lakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zakaria, kwa maana Mungu amesikia maombi yako. Mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita jina Yahya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Lakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zekaria, kwa maana Mwenyezi Mungu amesikia maombi yako. Mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yahya.

Tazama sura Nakili




Luka 1:13
27 Marejeleo ya Msalaba  

Nae atazaa mtoto mwanamume, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, ndiye atakaewaokoa watu wake na dhambi zao.


Marra Yesu akasema nao, akinena, Jipeni moyo; ni mimi; msiogope.


Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnanitafuta Yesu aliyesulibiwa.


Nae akawaambia, Msistaajabu; muamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa: amefufuka: bayupo hapa: patazameni pahali walipomweka.


Nawe utakuwa na furaha na shangwe; na watu wengi watafurahia kuzaliwa kwake.


Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu; kwa maana umepata neema kwa Mungu.


Na zilipotimia siku nane za kumtahiri, alikwitwa jina lake Yesu, lile lililotajwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.


Kornelio, maombi yako yamesikiwa, na sadaka zako zinakumbukwa mbele za Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo