Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Filemoni 1:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 illi ushirika wa imani yako ufanye kazi yake katika ujuzi wa killa kitu chema kilicho kwenu katika Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Naomba ili imani hiyo unayoshiriki pamoja nasi ikuwezeshe kuwa na ujuzi mkamilifu zaidi wa baraka zote tunazopata katika kuungana kwetu na Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Naomba ili imani hiyo unayoshiriki pamoja nasi ikuwezeshe kuwa na ujuzi mkamilifu zaidi wa baraka zote tunazopata katika kuungana kwetu na Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Naomba ili imani hiyo unayoshiriki pamoja nasi ikuwezeshe kuwa na ujuzi mkamilifu zaidi wa baraka zote tunazopata katika kuungana kwetu na Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Naomba utiwe nguvu katika kushiriki imani yako na wengine, ili upate kuwa na ufahamu mkamilifu wa kila kitu chema tunachoshiriki kwa ajili ya Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Naomba utiwe nguvu katika kuishuhudia imani yako, ili upate kuwa na ufahamu mkamilifu juu ya kila kitu chema tulicho nacho ndani ya Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




Filemoni 1:6
18 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi yule aliyepokea talanta tano akashika njia, akafanya kazi nazo, akachuma talanta nyingine tano.


Vivi hivi nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wakamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.


na hivyo siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo, akianguka kifudifudi, atamwabudu Mungu, akikiri ya kuwa Mungu yu kati yenu hila shaka.


kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wengi wako wanipingao.


Khatimae, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya heshima, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye kuvuma vizuri, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini haya.


Kwa sababu hiyo na sisi, tangu siku tuliposikia, hatuachi kuwaombeeni, na kuomba dua, mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;


mkamvaa mtu mpya anaefanywa upya apate maarifa kwa mfano wake yeye aliyemumba.


Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema kwa matumizi yaliyo lazima, illi wasiwe hawana matunda.


maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia.


Yafaa nini, ndugu zangu, mtu akisema ana imani, nae hana matendo? Je! ile imani yaweza kumwokoa?


Vivyo hivyo na imani, isipokuwa na matendo, imekufa nafsini mwake.


mwe na maongezi mazuri kati ya Mataifa, illi, iwapo huwasingizia kuwa mnatenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa nae.


KADHALIKA ninyi wake, watumikieni waume o zenu; kusudi, ikiwa wako waume wasioliamini Neno, kwa mwenendo wa wake zao, pasipo Neno lile, wavutwe;


mkiwa na dhamiri njema, illi katika neno lile mnalosingiziwa kwamba m watenda mabaya, wataha yarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.


Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo