Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Yohana 1:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Na sasa, Bibi, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Basi, Bimkubwa, ninalo ombi moja kwako: Tupendane. Ombi hili si amri mpya, bali ni amri ileile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Basi, Bimkubwa, ninalo ombi moja kwako: Tupendane. Ombi hili si amri mpya, bali ni amri ileile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Basi, Bimkubwa, ninalo ombi moja kwako: tupendane. Ombi hili si amri mpya, bali ni amri ileile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Sasa, mama mteule mpendwa, si kwamba ninakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo. Tupendane kila mmoja na mwenzake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Sasa, bibi mpendwa, si kwamba ninakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo. Tupendane kila mmoja na mwenzake.

Tazama sura Nakili




2 Yohana 1:5
17 Marejeleo ya Msalaba  

Amri yangu ndio hii, mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.


Haya nawaamuru, mpate kupendana.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri.


Kwa khabari ya upendano, hamna haja niwaandikie: maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.


zaidi ya yote mwe na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husetiri wingi wa dhambi;


na katika utawa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.


Maana hii ndiyo khabari tuliyosikia tangu mwanzo, tupendane sisi kwa sisi;


Na hii ndiyo amri yake, tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana, kama alivyotupa amri.


Mtu akisema, Nampenda Mungu, nae anamchukia ndugu yake, yu mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambae amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambae hakumwona.


MZEE kwa bibi mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na ndugu wote waijuao ile kweli;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo