Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wathesalonike 3:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Twawaagizeni, ndugu, katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na killa ndugu aendae bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Ndugu, tunawaamuru kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mjiepushe na ndugu wote walio wavivu na ambao hawafuati maagizo tuliyowapa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Ndugu, tunawaamuru kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mjiepushe na ndugu wote walio wavivu na ambao hawafuati maagizo tuliyowapa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Ndugu, tunawaamuru kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mjiepushe na ndugu wote walio wavivu na ambao hawafuati maagizo tuliyowapa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Ndugu, tunawaagiza katika Jina la Bwana Isa Al-Masihi, jitengeni na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Ndugu, tunawaagiza katika Jina la Bwana Isa Al-Masihi, jitengeni na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapa.

Tazama sura Nakili




2 Wathesalonike 3:6
24 Marejeleo ya Msalaba  

Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa: na asipolisikiliza kanisa pia, na awe sawasawa na mtu wa Mataifa na mtoza ushuru.


Nawasihini, ndugu, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.


Tena nawasifu, ndugu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale niliyowatolea vile vile kama nilivyowatolea.


Katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na nweza wa Bwana wetu Yesu Kristo,


Naliwaandikieni katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi.


Maana kama mkimsamehe mtu lo lote, na mimi; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele ya Kristo,


Bassi nasema neno bili, tena nashuhudu katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waendavyo, katika ubatili wa nia zao,


Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.


ILIYOBAKI, ndugu, tunakusihini na kukuonyeni kuenenda katika Bwana Yesu, kama mlivyopokea kwetu, jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama na muavyoenenda, mpate kuzidizidi sana.


tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe kama tulivyowaagiza;


Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.


Bassi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ikiwa kwa maneno, au kwa waraka wetu.


Mwajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata, kwa sababu hatukwenda bila utaratibu kwenu;


Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Bwana Kristo Yesu, na mbele ya malaika wateule, yatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.


na majadiliano ya watu walioharibiwa akili zao, walioikosa kweli, wakidhani ya kuwa utawa ni njia ya kupata faida; ujitenge na watu kama hao,


wenye mfano wa utawa, lakini wakikana nguvu zake; ujiepushe na hao.


NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake;


Mtu akija kwenu, nae haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo