Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wathesalonike 3:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 tukaokolewe na watu wasio haki, wahaya; maana si wote walio na imani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Ombeni pia ili Mungu atuokoe na watu wapotovu na waovu, maana si wote wanauamini ujumbe huu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Ombeni pia ili Mungu atuokoe na watu wapotovu na waovu, maana si wote wanauamini ujumbe huu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Ombeni pia ili Mungu atuokoe na watu wapotovu na waovu, maana si wote wanauamini ujumbe huu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Ombeni pia ili tupate kuokolewa kutokana na watu waovu na wabaya, kwa maana si wote wanaoamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Ombeni pia ili tupate kuokolewa kutokana na watu waovu na wabaya, kwa maana si wote wanaoamini.

Tazama sura Nakili




2 Wathesalonike 3:2
18 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini na kipotofu, nitakuwa pamoja nanyi hatta lini? Nitachukuliana nanyi hatta lini? Mleteni huku kwangu.


Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnalipa zaka za mnaana na bizari na kumini, mkaacha mambo makuu ya sharia, hukumu, na rehema, na imani: haya imewapasa kuyafanya, na mengine yale msiyaache.


Walakini Mwana wa Adamu atakapokuja, je! ataiona imani duniani?


Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana.


Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watawa na watu wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paolo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.


Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu.


Na Wayahudi wasioamini wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yason wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;


Kwa maana naona ni neno lisilo maana kumpeleka mfungwa, bila kuonyesha mashitaka yale aliyoshitakiwa.


Wengine waliamini yaliyonenwa, wengine hawakuyaamini.


Lakini si wote walioitii khahari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, nani aliyeamini khabari zetu?


niokolewe nao waasio katika Yahudi, na tena khuduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemi ipate kibali kwa watakatifu,


Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na nyama wakali kule Efeso, nina faida gani wasipofufuka wafu? Tule, tukanywe, maana kesho tutakufa.


Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paolo, marra ya kwanza, na marra ya pili. Shelani akatuzuia.


Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, illi kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, mataifa wrote wakasikie; nikaokolewa katika kanwa la simba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo