Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wathesalonike 2:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambae Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mafunuo ya kuwako kwake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Hapo ndipo Mwovu atakapotokea; lakini Bwana Yesu anapokuja atamuua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa mngao wa kuja kwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Hapo ndipo Mwovu atakapotokea; lakini Bwana Yesu anapokuja atamuua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa mngao wa kuja kwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Hapo ndipo Mwovu atakapotokea; lakini Bwana Yesu anapokuja atamuua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa mng'ao wa kuja kwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Isa atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Isa atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake.

Tazama sura Nakili




2 Wathesalonike 2:8
34 Marejeleo ya Msalaba  

Killa alisikiae neno la ufalme asifahamu, huja yule mwovu, akaliteka lililopandwa moyoni mwake. Huyu ndiye aliyepandwa njiani.


na lile konde ni ulimwengu; na zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;


Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.


nae alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, na vitu ambavyo haviko, illi avibatilishe vilivyoko;


Mtu aliye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana haiji isipokuja kwanza ile faraka, akafumiliwa yule mtu wa dhambi, mwana wa uharibifu,


ilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hatta kudhihiri kwake Bwana wetu Yesu Kristo,


na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Yesu Kristo, aliyebatili mauti na kuufunua uzima ua kutoa kuharibika, kwa ile Injili,


NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake;


baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.


tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo;


bali kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.


Nawaandikia, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nawaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba.


si kama Kain alivyokuwa wa yule Mwovu, akamwua ndugu yake. Nae alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake ya haki.


Twajua ya kuwa killa mtu aliyezaliwa na Mungu hakosi: bali yeye aliyezaliwa na Mungu ajilinda, na yule mwovu hamgusi.


Nae alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume: na upanga mkali, mkali kuwili, watoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua likingʼaa kwa nguvu zake.


Akapewa kinywa kunena maneno makuu, ya ukafiri. Akapewa uwezo kufanya kazi yake miezi arubaini na miwili.


Na upanga mkali hutoka kinywani mwake awapige mataifa kwa huo. Nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, nae anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ukali wa ghadhabu ya Mungu Mwenyiezi.


Tubu; na usipotubu naja kwako upesi, nitafanya vita juu yako kwa upanga wa kinywa changu.


Na yule Msingiziaji, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule nyama na yule nabii wa nwongo. Na wataumwa mchana na usiku hatta milele na milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo