Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wathesalonike 2:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, illi kuupata ntukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Mungu aliwaitieni jambo hili kwa njia ya Habari Njema tuliyowahubirieni; aliwaiteni mpate kupokea sehemu yenu katika utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Mungu aliwaitieni jambo hili kwa njia ya Habari Njema tuliyowahubirieni; aliwaiteni mpate kupokea sehemu yenu katika utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Mungu aliwaitieni jambo hili kwa njia ya Habari Njema tuliyowahubirieni; aliwaiteni mpate kupokea sehemu yenu katika utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kwa kusudi hili Mungu aliwaita ninyi kupitia Injili tuliyowahubiria, ili mpate kushiriki katika utukufu wa Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kwa kusudi hili Mungu aliwaita kwa njia ya kuhubiri kwetu Injili, ili mpate kushiriki katika utukufu wa Bwana Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




2 Wathesalonike 2:14
19 Marejeleo ya Msalaba  

Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema, na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako.


Nami, utukufu ule ulionipa nimewajia wao, wawe umoja, kama sisi tulivyo umoja:


Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wana Adamu, sawa sawa na injili yangu, kwa Yesu Kristo.


kama tu watoto, bassi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja nae illi tutukuzwe pamoja nae.


macho ya akili zenu yakitiwa nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo,


kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthubutifu mwingi; kama mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.


illi mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Mungu mwenende, awaitae muingie katika ufalme wake na utukufu wake.


kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi:


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


kwa kuwa uweza wa Mungu umetukarimia vitu vyote vyenye uzima na utawa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe;


Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi uuangaze, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana kondoo.


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo