Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wathesalonike 2:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokofu, katika kutakaswa kwa Roho na kuiamini kweli,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu nyinyi ndugu, nyinyi mnaopendwa na Bwana, kwa maana Mungu amewateua tangu mwanzo mpate kuokolewa kwa nguvu ya Roho, mfanywe watu wake watakatifu kwa imani yenu katika ukweli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu nyinyi ndugu, nyinyi mnaopendwa na Bwana, kwa maana Mungu amewateua tangu mwanzo mpate kuokolewa kwa nguvu ya Roho, mfanywe watu wake watakatifu kwa imani yenu katika ukweli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu nyinyi ndugu, nyinyi mnaopendwa na Bwana, kwa maana Mungu amewateua tangu mwanzo mpate kuokolewa kwa nguvu ya Roho, mfanywe watu wake watakatifu kwa imani yenu katika ukweli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Lakini inatupasa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana Isa, kwa sababu Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho wa Mungu kwa kuiamini kweli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mwenyezi Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana Isa, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho wa Mwenyezi Mungu kwa kuiamini kweli.

Tazama sura Nakili




2 Wathesalonike 2:13
42 Marejeleo ya Msalaba  

Katika utakatifu na kwa haki mbele zake siku zetu zote.


MWANZO alikuwako Neno, nae Neno alikuwako kwa Mungu, nae Neno alikuwa Mungu.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.


wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani.


Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;


Ni nani atakaewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye awahesabiae haki.


kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, illi lisimame kusudi la Mungu la kuchagua,


Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalokhubiriwa.


ENYI Wagalatia msio akili, ni nani aliyewaloga, msiisadiki kweli, ninyi ambao Kristo aliwekwa mbele ya macho yemi ya kuwa amesulibiwa?


Maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu:


kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, khabari zake mlisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;


Bassi, kwa kuwa mu wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, vaeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,


tukijua, ndugu mnaopendwa na Mungu, uteule wenu,


illi mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Mungu mwenende, awaitae muingie katika ufalme wake na utukufu wake.


Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.


Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira vake bali tupate wokofu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo,


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


na katika madanganya yote ya udhalimu kwao wanaopotea: kwa sababu hawakukubali kuipenda kweli, wapate kuokolewa.


illi wahukumiwe wote wasioamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.


Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,


aliyetuokoa akatuita kwa wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa sisi katika Kristo Yesu, kabla ya nyakati za zamani;


Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiyetahayarishwa, ukitumia kwa halali neno la Mungu.


na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, yawezayo kukuhekimisha hatta upate wokofu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.


Na, wewe, Bwana, mwanzo umeitia misingi ya inchi, na mbingu ni kazi za mikono yako;


Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake.


Hili ndilo pendo, si kwamba sisi twalimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akampeleka Mwana wake kuwa kipatanislio kwa dhambi zetu.


Sisi twapenda kwa maana yeye kwanza alitupenda sisi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo