Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wathesalonike 1:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 ndio ishara ya hukumu ya haki ya Mungu illi mstabilishwe kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Hayo yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na matokeo yake, nyinyi mtastahili ufalme wake ambao kwa ajili yake mnateseka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Hayo yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na matokeo yake, nyinyi mtastahili ufalme wake ambao kwa ajili yake mnateseka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Hayo yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na matokeo yake, nyinyi mtastahili ufalme wake ambao kwa ajili yake mnateseka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili kuwa wa ufalme wa Mungu, mnaoteswa kwa ajili yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili kuwa wa Ufalme wa Mwenyezi Mungu, mnaoteswa kwa ajili wake.

Tazama sura Nakili




2 Wathesalonike 1:5
28 Marejeleo ya Msalaba  

bali wao watakaohesabiwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na ufufuo wa wafu, hawaoi wala hawaozwi,


Kwa hiyo kesheni killa wakati, mkiomba mpate kuhesabiwa kuwa mmestahili kuponea haya yote yatakayokuwa, na kusimama mahali penu mbele ya Mwana wa Adamu.


Paolo na Barnaba wakanena kwa uthabiti wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza: illakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, wala hamjioni nafsi zenu kuwa mmestahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia mataifa.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,


kama tu watoto, bassi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja nae illi tutukuzwe pamoja nae.


BASSI nawasihini, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa,


wala hamwogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara wazi ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokofu, nao wa Mungu.


mkimshukuru Baba, aliyetustahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru;


Maana uinyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu, waliyopata na hao kwa Wayahudi;


Kwa hiyo twawaombea ninyi siku zote, illi Mungu wetu awahesabu kuwa nimeustahili wito wenu, akatimize killa haja ya wema na killa kazi ya imani kwa nguvu:


kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi:


Ni nani asiyekucha, Bwana, na kulitukuza jina lako? kwa kuwa wewe peke yako Mtakatifu: kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele yako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.


Nikaisikia madhbahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyiezi, za kweli, za haki hukumu zako.


kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki: maana amemhukumu yule kahabu mkuu aliyeiharibu inchi kwa uasharati wake, na kumpatiliza kwa ajili va damu ya watumwa wake mkononi mwake.


Lakini unayo majina machache, hatta katika Sardi, watu wasioyatia uchafu mavazi yao. Nao watakwenda pamoja nami katika mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo