Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wathesalonike 1:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Hatta sisi wenyewe twajisifu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya uvumilivu wenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na mateso mnayoyavumilia;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Ndio maana sisi tunajivunia nyinyi katika makanisa ya Mungu. Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso mnayopata.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Ndio maana sisi tunajivunia nyinyi katika makanisa ya Mungu. Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso mnayopata.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Ndio maana sisi tunajivunia nyinyi katika makanisa ya Mungu. Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso mnayopata.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Ndiyo sababu miongoni mwa makundi ya waumini ya Mungu, tunajivunia saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Ndiyo sababu miongoni mwa makundi ya waumini ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili.

Tazama sura Nakili




2 Wathesalonike 1:4
24 Marejeleo ya Msalaba  

kwa tumaini, mkifurahi; katika shidda, mkivumilia; katika kusali, mkidumu;


wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;


Bali tukikitumaini kitu tusichokiona, twakingojea kwa uvumilivu.


Lakini Mungu alivyomgawia killa mtu—kama Mungu alivyomwita killa mtu, na aenende vivyo hivyo. Na ndivyo ninavyoagiza katika Makanisa yote.


Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na maumivu, na dhiiki, na adha, na shidda, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo ua nguvu.


Kwa maana, ikiwa nimejisifu kwake kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; hali, kama tulivyowaambieni mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli.


Nina ujasiri mwingi kwemi; kujisifu kwangu kwa ajili yenu ni kwingi. Nimejawa na faraja, katika mateso yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi.


Maana najua utajiri wenu, niliojisifia kwa Wamakedoni, kwamba Akaya ilikuwa tayari tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo watu wengi.


kusudi, wakija Wamakedoni pamoja nami, na kuwakuta hamjawa tayari, tusije tukatahayarika sisi, tusiseme ninyi, katika hali hii va kutumaini.


wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;


Maana uinyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu, waliyopata na hao kwa Wayahudi;


Maana tumnini letu, au furaha yetu, an taji ya kujisifu ni nini? Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu Kristo wakati wa kuja kwake?


Bwana awaongozeni mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na uvumilivu wa Kristo.


Maana mnahitaji uvumilivu, illi mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu muipate abadi.


illi msiwe wavivu, hali wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imaui na uvumilivu.


Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.


Angalieni, twawaita wenye kheri wao waliovumilia. Mmesikia khabari ya uvumilivu wa Ayub, mmenona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwenye rehema nyingi, mwenye huruma.


na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu uvumilivu, na katika uvumilivu wenu utawa,


Hapo ndipo penye uvumilivu wa watakatifu wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo