Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wathesalonike 1:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Kwa hiyo twawaombea ninyi siku zote, illi Mungu wetu awahesabu kuwa nimeustahili wito wenu, akatimize killa haja ya wema na killa kazi ya imani kwa nguvu:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Ndiyo maana tunawaombeeni daima. Tunamwomba Mungu wetu awawezesheni kustahili maisha aliyowaitia muyaishi. Tunamwomba, kwa uwezo wake, atimize nia yenu ya kutenda mema na kukamilisha kazi yenu ya imani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Ndiyo maana tunawaombeeni daima. Tunamwomba Mungu wetu awawezesheni kustahili maisha aliyowaitia muyaishi. Tunamwomba, kwa uwezo wake, atimize nia yenu ya kutenda mema na kukamilisha kazi yenu ya imani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Ndiyo maana tunawaombeeni daima. Tunamwomba Mungu wetu awawezesheni kustahili maisha aliyowaitia muyaishi. Tunamwomba, kwa uwezo wake, atimize nia yenu ya kutenda mema na kukamilisha kazi yenu ya imani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Kwa sababu hii, tunawaombea ninyi bila kukoma, ili Mungu wetu apate kuwahesabu kuwa mnastahili wito wake na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila kusudi lenu jema na kila tendo linaloongozwa na imani yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Kwa sababu hii, tunawaombea ninyi bila kukoma, ili Mwenyezi Mungu apate kuwahesabu kuwa mnastahili wito wake na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila kusudi lenu jema na kila tendo linaloongozwa na imani yenu.

Tazama sura Nakili




2 Wathesalonike 1:11
41 Marejeleo ya Msalaba  

Maana inchi huzaa yenyewe, kwanza jani, tena suke, kiisha nganu mpevu katika suke.


Msiogope, enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapeni ufalme.


Kwa maana Mungu, nimwabuduye kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake ni shahidi wangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma, siku zote katika sala zangu


Kwa sababu karama za Mungu na wito wake hazina majuto.


Na mimi mwenyewe, ndugu zangu, nimehakikishwa kwa khahari zenu kama ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana.


Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hawa akawatukuza.


na yeye atawathubutisheni hatta mwisho, msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.


siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu;


Kwa kuwa ametuchagua tangu zamani illi tufanywe waua wake yeye kwa njia ya Yesu Kristo, kwa mapenzi ya nia yake,


akiisha kutujulisha siri ya nia yake, kwa kadiri ya mapenzi yake, aliyoyakusudia katika yeye huyu,


niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hatta siku ya Yesu Kristo;


kwa maana ni Mungu atendae ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa ajili ya kusudi lake jema.


nakaza mwendo, niifikilie thawabu ya wito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.


wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;


ndio ishara ya hukumu ya haki ya Mungu illi mstabilishwe kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa;


aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, illi kuupata ntukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Lakini unayo majina machache, hatta katika Sardi, watu wasioyatia uchafu mavazi yao. Nao watakwenda pamoja nami katika mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.


ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa killa kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu: nao wanamiliki juu ya inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo