Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 9:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Mungu ashukuriwe kwa sababa ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu ipasavyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi yake isiyo na kifani!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi yake isiyo na kifani!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi yake isiyo na kifani!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Mungu apewe shukrani kwa karama yake isiyoelezeka!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Ashukuriwe Mungu kwa karama yake isiyoelezeka.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 9:15
23 Marejeleo ya Msalaba  

Utukufu una Mungu palipo juu, Na katika inchi amani, kwa watu aliowaridhia.


Akitokea yeye nae saa ileile, alimshukuru Mungu, akawapasha khabari zake watu wote waliokuwa wakitazamia ukombozi katika Yerusalemi.


Na katika ujazi wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.


Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hatta akampeleka Mwana wake wa pekee, illi mtu aliye yote amwaminiye asipotee, bali apate uzima wa milele.


Lakini kipawa kile hakikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kuanguka kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema ya mtu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.


Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja nae?


Lakini tumshukuru Mungu atupae kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


Mungu ashukuriwe, anaetushangiliza daima katika Kristo, na kuyadhihirisha manukato ya hawa wamjuao killa pahali kwa kazi yetu.


mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.


Nao wenyewe, wakiwaombea ninyi, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sanu ndani yenu.


mkimshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;


Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.


Na hawa nyama wenye uhayi watakapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi yeye aliye hayi hatta milele na milele ntukufu na heshima na shukrani,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo