Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Wakorintho 9:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huu, mnamtukuza Mungu kwa ajili ya ntii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Kutokana na uthibitisho unaooneshwa kwa huduma hii yetu, watu watamtukuza Mungu kwa sababu ya uaminifu wenu kwa Habari Njema ya Kristo mnayoiungama, na pia kwa sababu ya ukarimu mnaowapa wao na watu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Kutokana na uthibitisho unaooneshwa kwa huduma hii yetu, watu watamtukuza Mungu kwa sababu ya uaminifu wenu kwa Habari Njema ya Kristo mnayoiungama, na pia kwa sababu ya ukarimu mnaowapa wao na watu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Kutokana na uthibitisho unaooneshwa kwa huduma hii yetu, watu watamtukuza Mungu kwa sababu ya uaminifu wenu kwa Habari Njema ya Kristo mnayoiungama, na pia kwa sababu ya ukarimu mnaowapa wao na watu wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Al-Masihi, na kwa ukarimu wenu wa kuwashirikisha wao na watu wengine wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Al-Masihi, na kwa ukarimu wenu wa kushiriki pamoja nao na pia wengine wote.

Tazama sura Nakili




2 Wakorintho 9:13
27 Marejeleo ya Msalaba  

Vivi hivi nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wakamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.


Makutano wakimwona, wakastaajabu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu mamlaka ya jinsi hii.


Ya nini kuniita Bwana, Bwana, nanyi hamyatendi niyanenayo?


Kwa hiyo atukuzwa Baba yangu, mzae sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.


Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Bassi, Mungu amewajalia mataifa nao toba liletalo uzima.


Nao walipokwisha kuwaogofya tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu: kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka:


Lakini si wote walioitii khahari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, nani aliyeamini khabari zetu?


mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukarimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidii; mwenye kurehemu, kwa furaha.


niokolewe nao waasio katika Yahudi, na tena khuduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemi ipate kibali kwa watakatifu,


ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulika na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, illi waitii imani;


tukiangusha mawazo na kiila kitu kilichoinuka, kijiinuacho jun ya elimu ya Mungu; na tukifanya mateka fikara zote zipate kumtii Kristo:


Bassi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo nikafunguliwa mlango katika Bwana,


kwa khiari yao wenyewe walitoa vitu vyao; wakituomba pamoja na kutusihi tuipokee neema hii, na kushirikiana nao huku kuwakhudumia watakatifu.


Nao wenyewe, wakiwaombea ninyi, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sanu ndani yenu.


Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.


Fanya vita vile vizuri vya imani, shika uzima wa milele ulioitiwa, ukayaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.


Nakuagiza mbele za Mungu avipae vitu vyote uzima, na mbele za Kristo Yesu aliyeungama maungamo yale mazuri mbele ya Pontio Pilato,


Tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni amini;


Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana na watu; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


Bassi, iwapo tunae kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, tujashike sana maungamo yetu.


nae alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokofu wa milele kwa watu wote wanaomtii;


Bali ninyi m mzao mteule, ukubani wa kifaume, taifa takatifu, watu wa milki, mpate kutangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo