Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Wakorintho 8:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini, bali kwanza walijitoa nafsi zao, wakampa Bwana; kiisha wakatupa sisi pia, kwa mapenzi ya Mungu,

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Hilo lilikuwa jambo ambalo hatukulitazamia kabisa! Kwanza walijitolea wao wenyewe kwa Bwana, kisha wakajitolea wenyewe kwetu pia, kufuatana na mapenzi ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Hilo lilikuwa jambo ambalo hatukulitazamia kabisa! Kwanza walijitolea wao wenyewe kwa Bwana, kisha wakajitolea wenyewe kwetu pia, kufuatana na mapenzi ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Hilo lilikuwa jambo ambalo hatukulitazamia kabisa! Kwanza walijitolea wao wenyewe kwa Bwana, kisha wakajitolea wenyewe kwetu pia, kufuatana na mapenzi ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Wala hawakufanya tulivyotazamia, bali walijitoa wao wenyewe kwa Bwana Isa kwanza, na ndipo wakajitoa kwa ajili yetu kufuatana na mapenzi ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Wala hawakufanya tulivyotazamia, bali walijitoa wao wenyewe kwa Bwana Isa kwanza na ndipo wakajitoa kwa ajili yetu, kufuatana na mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

2 Wakorintho 8:5
15 Marejeleo ya Msalaba  

BASSI, nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, mtoe miili yenu iwe dhabihu hayi, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ibada yenu yenye maana.

wala msitoe viungo vyenu kuwa silaha ya dhulumu kwa dhambi; bali jitoeni nafsi zenu sadaka kwa Mungu kama walio hayi baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.

PAOLO, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,

Kwa maana hatujikhubiri nafsi zetu, hali Kristo Yesu Bwana; na sisi wenyewe kuwa watumishi wenu kwa ajili ya Kristo.

TENA twawaarifu ninyi, ndugu, kliahari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo